Wednesday, 2 July 2014

Video: T-Obay feat Iyanya - Commander

Msanii kutoka Chiggzy EntertainmentT-Obay ameachia video ya single yake mpya has dropped the visuals to his first single “Commander” featuring Iyanya

Dogo Janja arudi Tiptop baada ya kuomba msamaha

Msanii Dogo Janja ambae aliondokaTiptop kwa kishindo na kufanya kazi na Ustaz Juma na Musoma, amerejea tena kambini (Tiptop) baada ya kuona maisha ya mtaani ni magumu
Akielezea kurudi kwake ndani ya Tiptop Madee amesema 
"Mi nilipigiwa simu na babu tale pamoja na Fela kwamba Abduli amekuja, kama miezi miwili imepita, amekuja anasema mkae myamalize, mi nikawaambiwa aah mbona mi sina tatizo, kwasababu mi mbona naongea nae, kwasababu akiwa na tatizo lake ananitumia meseji ananiomba ushauri, sema tu kwa maswala hayo ya kazi sijawahi kuongea nae chochote.

kuna siku alifanya interview namillard alisema. alitubu mambo aliyokuwa anayaongea kwamba ulikuwa ni utoto, na kweli mi nikaangalia kwa haraka haraka umri aliokuwa nao mwanzo na sasa hivi ni vitu viwili tofauti.
jana pia nikakuta hizo taarifa nikawaambia mbona mi sina tatizo, tukamuita maskani jana tukaongea nae fresh, basi mpaka sasa hivi tuko nae, lakini bado hakuna vitu vingi vinavyoendelea, bado mapema sana, tukishakuwa tayari tutawaambia, lakini ukweli ni kwamba Abduli, Dogo Janja amejoin tena kwenye connection yetu , hicho ndio cha msingi, mengine yote tutawapa taarifa"

Dogo Janja pia nae pia alifunguka sababu za kurudi tena kwenye kambi yake aya mwanzo 

"kwasababu kwanza kuna vitu ambavyo namiss katika mziki wangu na pia nimemiss familia yangu ya mwanzo, kuna vitu ambavyo vinamiss katika mziki wangu hata watu wangu wanaona, nakuwa niko tofauti sana na mazingira ya mziki, sawa naweza kuwa na record sana lakini nyimbo naweka ndani tu, lakini tofauti na huku unapangiwa labda utatoa ngoma hii uutatoa ngoma hii hivyo tu"

kuhusu yeye na Ostaz Juma na Musoma

"Mkataba tu uliisha, tuko poa ila mkataba wangu mi na yeye uliisha, tuko fresh" amesema Dogo Janja


Baada ya ushindi wa Tuzo za BET Davido afanya callable na Meek Mill

 Katika kile alichokiandika mshindi wa Tuzo za BET "Davido" kutoka Nigeria hakuna shaka kuwa ameshafanya collable na msanii wa May Bach Music, Meek Mill.
Kupitia account yake ya instagram, davido alimuanidkia Meek Mill kuwa hawezi kusubiri kusikia kazi yao imetoka baada ya Mill kumpa hongera ya ushindi wa tuzo ya BET "Best International Act" Africa



Video: Watu wanne wafariki baada ya ndege iliyokuwa imebeba mirungi kuanguka jijini Nairobi

Crew member wanne wamefariki duniajumatano ya  leo asubuhi (July 2) baada ya ndege ya mizigo waliyokuwa wakisafiri nayo kugonga katika jengo lililoko Utawala, Embakasi.
UTAWALA-CRASH
Ndege hiyo ya mizigo iliyokuwa ikisafirisha mirungi kuelekea Mogadishu ilikuwa na watu watutu, iligomga jengo la biashara lililopo Utawala wakati ilipokuwa ikiondoka katika uwanja wa ndege wa KIA (Kenya International Airport)

Jengo lililogongwa na ndege hiyo halikuwa na watu kwasababu ilikuwa ni mapema sana, ambapo  Chief Police Benson Kibui amethibitisha ndege hiyo kunyanyuka mida ya saa kumi za alfajiri.
Mpiga picha aliekuwa katika eneo la tukio, amesema ndege iligonga jengo hilo lililo na viduka vidogo vidogo kilometa tatu kutoka airport
watu wote wanne waliokuwakatika ndege hiyo wamefariki dunia

Brand New Single: Sio Fair - Baraka Da Prince

Baraka Da Prince, msanii alieingia kwa kasi katika mziki wa Bongo Fleva Tanzania, amerudi na ujio wa pili baada ya kufanya poa na pini lake la kwanza "Jichunge".


Baraka ambae anatoka jiji la Mwanza kwa sasa amekuja na ngoma mpya "Sio Fair" iliyofanyika studio za tetemesha iliyopo Mwanza.
Sio Far imetengenezwa na kusimamiwa na ma producer watatu ambao ni Kid boy, Nusder na Lollypop


Video: Interview ya Vanessa Mdee na AM live cha NTV Kenya

Siku kadhaa zilizopita mwanamuziki na Mtangazaji Vanessa mdee alikuwa nchini Kenya kwa ajili ya kutambulisha wimbo wake mpya "Hamjui" na kufanikiwa kufanya interviews katika station mbali mbali.
Moja kati ya vituo vilivyofanya nae mahojiano ni pamoja na kipindi cha TV cha AM kinachoruka kupitia NTV....


Tuesday, 1 July 2014

Davido, Tiwa Savage na Ice Prince wahojiwa na kipindi cha TV cha P Diddy

mshindi wa tuzo za BET "International Act" Africa, Davido na nominee Tiwa Savage leo hii wamehojiwa na kipindi cha TV cha network ya P Diddy "Revolt
Katika interview hiyo, mkali wa hit ya "Aye" ameonekana akiwa katika kofia pamoja na tshirt ya leather, jeans ya denim na cheni kibao za gold wakati Tiwa akiwa ametupia kigauni cha pink na viatu virefu vya neon, Christian Louboutin.


Tiwa Savage

Ice Prince

TID kwa Ray C: you drug addicted, you been doing alot of shit, you been staying in ghettos,i don't want influence yangu ikawa mbaya

Tangu jana usiku mpaka leo hii , story ya TID na Ray C imekuwa gumzo kupitia social media zote
, wengine wakimshutumu TID kwa kutoa majibu ya kashfa na matusi kwa Ray C huku wengine wakiona ni sawa alichokiandika TID kwa kudai Ray C hakutakiwa kumuaandikia comment hiyo katika account ya Instagram ambayo iko public  


Kupitia 255 ya XXL leo TID amefunguka zaidi na hiki ndicho alichokisema

"Aaah kumbe ni yeye ndio ananitafuta, why cant you just call her halafu ndo unipigie mimi simu, umwambie kwanini unamtafuta huyu jamaa na kwanini na kwanini, kwasababu mimi kama mtu ananitafuta hawezi kunitafuta kwenye instagram, so may be she is trying to make somebody happy, sasa ndo hicho ambacho kime,  umeona labda kuna tatizo.



sijawahi kuwa na matatizo na Ray c mimi hata sijawahi yaani, kwanza sijamuona kama miaka mitano, nashangaa,nini anataka kuongea na mimi Ray C, mbona hajanitafuta miaka yote anitafute saa hivi, if she wanna make a point out of it, i really dont like it yaani wewe sasa nakwambia jamaa hataki kuonana na wewe you drug addicted, you been doing alot of shit, you been staying in ghettos, you been being a prostitute, so me i don't want influence yangu ikawa mbaya, kwahiyo staki kuongea nae staki kukutana nae, akaongee na ma boyfriend zake anaofanya nao vitu vibaya, am not her type, mimi am living with my family, am living with my mum, i drive my cars, come on man, 
am not her type, umeelewa, she wants to prove a point, may be she wants to make up with me, am not ready my friend, i don't date women like her, umeelewa, yaani kama anataka back up, asitafute backup kwangu, kuna society kibao ambazo anaweza kuzisaidia, anaweza akashuka pale kinondono manyanya akafanya nini, kwa hiyo she shouldn't be involved na mambo yangu na maisha yangu, awasaidie watu wengine, mimi i really don't need to see her kabisa, she is a bad influence " amesema TID

Beyonce Knowles aongoza orodha ya watu 100 waliongiza mkwanja na maarufu duniani

Beyonce Knowles, ameongoza nafasi ya kwanza katika list ya watu 100 maarufu duniani kwa mujibu wa Forbes 
Forbes wamefanikiwa kutengeneza list hiyo baada ya kufatilia mkwanja walioingiza tangu June 2013 mpaka June 2014 na pia umaarufu wa watu hao kupitia mitandao ya kijamii, radio pamoja na television kujua ni mara ngapi wamekuwa wakitajwa.
Beyonce amemtoa Oprah kutoka katika nafasi hiyo ya kwanza ambayo aliishika mwaka jana, na kumpeleka mpaka nafasi ya nne mwaka huu, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na mcheza kikapu Lebron James.
mwaka wa mafanikio makubwa sana kwa Beyonce hasa kwa tuwa kubwa aliyoifanya, Muimbaji nyota huyo alipiga show 95 na kuingiza wastani wa dola milioni 2.4 kwa kila mji, kwa mujibu wa pollstar.
Beyonce pia ameachia album yake mpya "Beyonce"  December bila promo yoyote, single "Drunk in love"  tayari mpaka sasa imeshauza zaidi ya kupi milioni moja.
Nafasi ya 2 imeshikiliwa na mcheza kikapu Lebron James, 3 ni Dr Dre, nafasi ya 4 imeshikiliwa na Oprah Winfrey, Nafasi ya 5 imechukuliwa na Mtangazaji Ellen Degeneres, huku Jay Z akiwa ameshika nafasi ya 6

Mshkaji wa karibu na 50 Cent, Floyd Mayweather Jr ameshika nafasi ya saba, huku Rihanna akiwa nafasi ya 8, Katy Perry amekamata nafasi ya 9 huku ya kumi ikiwa imehukuliwa na Robert Downey Jr muigizaji wa movie ambae mkwanja mwingi ameingiza mwaka huu kupitia "The Irone Man 3"

Monday, 30 June 2014

Trending tonight: Comment ya Ray C kumtaka Tid kuongea nae yamcharua Myama

Kikubwa kinachoendelea usiku huu, ni majibu aliyoyatoa TID kwa msanii mwenzake na mwanaharakati katika kukomesha matumizi ya madawa ya kulevya Ray C.
Ingawa haijajulikana rasmi ni nini kilicho muudhi Mzee Warioba a.k.a TID, katika comment aliyoiandika Ray C katika moja ya picha zake alizozituma Instagram
"Come lets talk Tid ur the best musician in east Africa pls lets talk"
TID alionekana kukerwa na Comment hiyo na kumpa makavu Ray C kwa kumtusi right under her comment




Sunday, 29 June 2014

Hiki ndicho alichokiandika Diamond kwa Watanzania baada ya kukosa tuzo ya BET

Ikiwa ni dakika chache tu baada ya kutangazwa Davido kuwa mshindi wa tuzo aliyokuwa akiiwania Diamond pia, Diamond amechukua muda wake na kuandika maneno haya kwa watanzania na wote wanao toa sapoti kwake




Davido anyukuwa tuzo iliyokuwa ikiwaniwa pia na Diamond

katika siku ambazo zilikuwa zikisubiriwa kwa hamu sana na watanzania pamoja na Africa kwa ujumla, ni leo ambapo tuzo za BET zinafanyika
Furaha ya watanzania ilianza tangu Diamond Platnumz alipochaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha "Best International Act" ambapo alikuwa akishindana na wasanii wengine akiwemo Davido.


bahati haikuwa ya watanzania kwamara nyingine kama ilivyokuwa katika tuzo za MAMA, na safari hii pia Davido ameondoka na tuzo hiyo .

akionyesha furaha yake kupitia acc yake ya Instagram Davido ameandika



video Teaser: Iyanya atupia video teaser ya wimbo alioshirikishwa na Diamond - Bum Bum

Video Teaser ya wimbo mpya wa Diamond akiwa amemshirikisha Iyanya kutoka Nigeria imeshatoka
Kupitia ukurasa wa Iyanya Instagram alipost video hiyo ambayo imerikodiwa uingereza.
Diamond alifanya collable hiyo na iyanya alivyokuja Bongo na kuimalizia nchini Nigeria lipoenda kwa ajili ya kuzindua wimbo wa kampeni ya kilimo (One Campaign)
tazama video hiyo hapa chini 


Saturday, 28 June 2014

Romantic Cascade Braid


How To :
- Make a dramatic side part on the far left side.
- Beginning at the side part, French braid along the front of the hairline, moving towards the right ear.
- Continue to braid, weaving in more and more hair as your work towards your right ear. Stop braiding just behind the right ear and secure with a dark or clear elastic.
- Take the remaining loose hair and curl 1-2" sections with a large barrel curling iron or a flat iron.* Gently run your fingers through curls to separate.
- To finish the look, wrap curls around bottom of braid to cover the elastic.
- Add a light mist of hairspray. And your done!

    Source : Hair dos: How to create a romantic cascade braided headband with curls

    Styling a Hair Bow Tutorial

    How To :
    - Brush your pretty locks.
    - Make half a pony tail by using a small hair tie.
    - take your pony tail halfway trough the hair tie, to create a 'loop'.
    - Split the loop in half.
    - Grab the leftover piece of hair, and fold it over the middle.
    - Secure with a bobby pin.
    - Make sure that you can't see the bobby pin.
    - Take one of the 'loops' and spread it over the side of your head. Slide a bobby pin through the middle of the loop. Repeat this on the other side.

      Source : Hair Bow DIY

      Quick & Easy Updo Hair Tutorial


      steps :
      Step 1 : Divide hair into three sections, the majority of your hair ending up in the low ponytail at the back of your head.
      Step 2 : Loosely braid the ponytail and secure it at the bottom.
      Step 3 : Tuck the bottom of the braid under the elastic securing the top of the braid, then pin the loop that forms to your head.
      Step 4 : Use the extra hair on the left and right sides of your head to wrap around the braid. You can twist them as much or as little as you like. Secure with more bobby pins.


      Source : Quick And Easy Updo Tutorial

      Friday, 27 June 2014

      Brand New Single: Sanaa Iko Sokoni - Illmatix feat Fid Q

      Illmatix, kundi linalosimamiwa na J mader kutoka Tongwe Record wameachia bonge la Hiphop Exclusive kupitia kipindi cha So So Fresh 
      Sanaa Iko Sokoni ni single yao mpya wakiwa wamemshirikisha Fid Q, sitaki kuongea mengi..sikiliza mwenye hapa chini 



      Exclusive Brand New Video: Unanichora - Ben Pol feat Joh Makini

      Leo ni siku nzuri sana kwa mwanamuziki Ben Pol, ameachia single mpya "Upendo" na video mpya "unanichora" aliyomshirikisha Joe Mkani
      Video imesimamiwa na Director Nisher, ambae amefanya nae kazi kwa mara ya pili, ya kwanza ni pale alipotengeneza pia video ya Jikubali.
      Ben Pol amesema kufanya kwake kazi na Nisher kwa mara ya pili ni kutokana na chemistry aliyonayo kati yake na Nisher, lakini pia amesema Nisher ni mtu ambae bado anajifunza, kwahiyo kuna vitu anaweza kugusa vikashangaza watu, na pia ni mtu ambae anasikiliza pia mteja wake anataka nini, kwa kifupi sio mjuaji.. tazama video hiyo hapa chini 


      Video: Wimbo mpya wa Ben Pol waleta mtafaruku kati ya Adam Mchomvu na Fetty

      Baada ya kuutambulisha wimbo mpya wa Ben Pol "Upendo" exclusive kupitia kipindi cha XXL kinachoendeshwa na B12, Fetty na Adam Mchomvu, kumetokea na ubishani kati ya Adam na Fetty juu ya wimbo huo ambao unamuonekano tofauti na jinsi alivyozoeleka Ben Pol
      Huku Fetty akiusifia na kuona ni wimbo wenye tofauti nzuri ambao una mahadhi ya bolingo na hata kusema ni fusion zinazotakiwa kwa sasa, Adam alionekana kuto kukubaliana nae na Ben Pol na kudai ni wimbo ambao sio mzuri kulinganisha na nyimbo zilizozoeleka kutoka kwa Ben Pol... 
      sikiliza kilichojiri leo hii kati ya watangazaji hao wawili



      Brand New Video: Nitasubiri - Jux

      Msanii mwenye Swag na muonekano wa Trey Song kuanzia sura, mwili mpaka tattoo, Jux , ameachia video ya wimbo wake "Nitasubiri" ulio rikodiwa nchini China.
      Baada ya kuuzinduwa Billcanas wiki kadhaa zilizopita, pata nafasi ya kuutizama hapa



      Brand New Song: Pita Mbele - Kiba Square

      Baada ya kile alichokidai ni kujifunza kuwa baba pamoja na kumuachia nafasi ya kukua ki muziki mdogo wake "Abdu Kiba", Ally kiba amerudi tena kwa ngoma ya kushirikiana na mdogo wake huyo "Pita Mbele"
      Wakiitambulisha rasmi single hiyo leo hii kupiti XXL, alikiba amesema "kuna Ally kiba na kuna Abdu Kiba, lakini Kiba Square ni katika kukata kiu ya mashabiki wengi ambao wamekuwa wakituomba kufanya kazi pamoja, lakini baada ya wiki kadhaa nitatoa wimbo wangu mwenyewe ambao unaitwa Dar-es-salaam" amesema Ally Kiba...sikiliza wimbo huo hapa chini 


      Brand New Single: Ben Pol - Upendo

      Mkali wa R&B Bongo Ben Pol a.k.a Ben Pizeeee, leo amedondosha single mpya "Upendo" aliyoifanya kwa producer Man Walter 
      Ben Pol amesema huu ndio wimbo wake wa kwanza kuandikiwa kuanzia mashairi mpaka melody ya wimbo huo na jamaa anaeitwa Kinye Wynjones. Katika wimbo huu Ben Pol amekuja kitofauti sana na jinsi tulivyomzoea. 

      dizaini kama bolingo flani hivi...msikilize hapo chini na usisahau kuwa leo hii utapata kuona video ya wimbo wake aliofanya na Joe Makini "Unanichora" ikifika saa nne za usiku hapa hapa kwa blog yako