Msanii kutoka Chiggzy Entertainment, T-Obay ameachia video ya single yake mpya has dropped the visuals to his first single “Commander” featuring Iyanya
Wednesday, 2 July 2014
Dogo Janja arudi Tiptop baada ya kuomba msamaha
Msanii Dogo Janja ambae aliondokaTiptop kwa kishindo na kufanya kazi na Ustaz Juma na Musoma, amerejea tena kambini (Tiptop) baada ya kuona maisha ya mtaani ni magumu
Akielezea kurudi kwake ndani ya Tiptop Madee amesema
"Mi nilipigiwa simu na babu tale pamoja na Fela kwamba Abduli amekuja, kama miezi miwili imepita, amekuja anasema mkae myamalize, mi nikawaambiwa aah mbona mi sina tatizo, kwasababu mi mbona naongea nae, kwasababu akiwa na tatizo lake ananitumia meseji ananiomba ushauri, sema tu kwa maswala hayo ya kazi sijawahi kuongea nae chochote.
kuna siku alifanya interview namillard alisema. alitubu mambo aliyokuwa anayaongea kwamba ulikuwa ni utoto, na kweli mi nikaangalia kwa haraka haraka umri aliokuwa nao mwanzo na sasa hivi ni vitu viwili tofauti.
jana pia nikakuta hizo taarifa nikawaambia mbona mi sina tatizo, tukamuita maskani jana tukaongea nae fresh, basi mpaka sasa hivi tuko nae, lakini bado hakuna vitu vingi vinavyoendelea, bado mapema sana, tukishakuwa tayari tutawaambia, lakini ukweli ni kwamba Abduli, Dogo Janja amejoin tena kwenye connection yetu , hicho ndio cha msingi, mengine yote tutawapa taarifa"
Dogo Janja pia nae pia alifunguka sababu za kurudi tena kwenye kambi yake aya mwanzo
"kwasababu kwanza kuna vitu ambavyo namiss katika mziki wangu na pia nimemiss familia yangu ya mwanzo, kuna vitu ambavyo vinamiss katika mziki wangu hata watu wangu wanaona, nakuwa niko tofauti sana na mazingira ya mziki, sawa naweza kuwa na record sana lakini nyimbo naweka ndani tu, lakini tofauti na huku unapangiwa labda utatoa ngoma hii uutatoa ngoma hii hivyo tu"
kuhusu yeye na Ostaz Juma na Musoma
"Mkataba tu uliisha, tuko poa ila mkataba wangu mi na yeye uliisha, tuko fresh" amesema Dogo Janja
its more about music industry and social issues in and out of bongo land
Baada ya ushindi wa Tuzo za BET Davido afanya callable na Meek Mill
Katika kile alichokiandika mshindi wa Tuzo za BET "Davido" kutoka Nigeria hakuna shaka kuwa ameshafanya collable na msanii wa May Bach Music, Meek Mill.
Kupitia account yake ya instagram, davido alimuanidkia Meek Mill kuwa hawezi kusubiri kusikia kazi yao imetoka baada ya Mill kumpa hongera ya ushindi wa tuzo ya BET "Best International Act" Africa
its more about music industry and social issues in and out of bongo land
Video: Watu wanne wafariki baada ya ndege iliyokuwa imebeba mirungi kuanguka jijini Nairobi
Crew member wanne wamefariki duniajumatano ya leo asubuhi (July 2) baada ya ndege ya mizigo waliyokuwa wakisafiri nayo kugonga katika jengo lililoko Utawala, Embakasi.
Ndege hiyo ya mizigo iliyokuwa ikisafirisha mirungi kuelekea Mogadishu ilikuwa na watu watutu, iligomga jengo la biashara lililopo Utawala wakati ilipokuwa ikiondoka katika uwanja wa ndege wa KIA (Kenya International Airport)
Jengo lililogongwa na ndege hiyo halikuwa na watu kwasababu ilikuwa ni mapema sana, ambapo Chief Police Benson Kibui amethibitisha ndege hiyo kunyanyuka mida ya saa kumi za alfajiri.
Mpiga picha aliekuwa katika eneo la tukio, amesema ndege iligonga jengo hilo lililo na viduka vidogo vidogo kilometa tatu kutoka airport
watu wote wanne waliokuwakatika ndege hiyo wamefariki dunia
its more about music industry and social issues in and out of bongo land
Brand New Single: Sio Fair - Baraka Da Prince
Baraka Da Prince, msanii alieingia kwa kasi katika mziki wa Bongo Fleva Tanzania, amerudi na ujio wa pili baada ya kufanya poa na pini lake la kwanza "Jichunge".
Baraka ambae anatoka jiji la Mwanza kwa sasa amekuja na ngoma mpya "Sio Fair" iliyofanyika studio za tetemesha iliyopo Mwanza.
Sio Far imetengenezwa na kusimamiwa na ma producer watatu ambao ni Kid boy, Nusder na Lollypop
Baraka ambae anatoka jiji la Mwanza kwa sasa amekuja na ngoma mpya "Sio Fair" iliyofanyika studio za tetemesha iliyopo Mwanza.
Sio Far imetengenezwa na kusimamiwa na ma producer watatu ambao ni Kid boy, Nusder na Lollypop
its more about music industry and social issues in and out of bongo land
Video: Interview ya Vanessa Mdee na AM live cha NTV Kenya
Siku kadhaa zilizopita mwanamuziki na Mtangazaji Vanessa mdee alikuwa nchini Kenya kwa ajili ya kutambulisha wimbo wake mpya "Hamjui" na kufanikiwa kufanya interviews katika station mbali mbali.
Moja kati ya vituo vilivyofanya nae mahojiano ni pamoja na kipindi cha TV cha AM kinachoruka kupitia NTV....
its more about music industry and social issues in and out of bongo land
Tuesday, 1 July 2014
Davido, Tiwa Savage na Ice Prince wahojiwa na kipindi cha TV cha P Diddy
mshindi wa tuzo za BET "International Act" Africa, Davido na nominee Tiwa Savage leo hii wamehojiwa na kipindi cha TV cha network ya P Diddy "Revolt
Katika interview hiyo, mkali wa hit ya "Aye" ameonekana akiwa katika kofia pamoja na tshirt ya leather, jeans ya denim na cheni kibao za gold wakati Tiwa akiwa ametupia kigauni cha pink na viatu virefu vya neon, Christian Louboutin.
Tiwa Savage
Ice Prince
its more about music industry and social issues in and out of bongo land
TID kwa Ray C: you drug addicted, you been doing alot of shit, you been staying in ghettos,i don't want influence yangu ikawa mbaya
Tangu jana usiku mpaka leo hii , story ya TID na Ray C imekuwa gumzo kupitia social media zote
, wengine wakimshutumu TID kwa kutoa majibu ya kashfa na matusi kwa Ray C huku wengine wakiona ni sawa alichokiandika TID kwa kudai Ray C hakutakiwa kumuaandikia comment hiyo katika account ya Instagram ambayo iko public
Kupitia 255 ya XXL leo TID amefunguka zaidi na hiki ndicho alichokisema
"Aaah kumbe ni yeye ndio ananitafuta, why cant you just call her halafu ndo unipigie mimi simu, umwambie kwanini unamtafuta huyu jamaa na kwanini na kwanini, kwasababu mimi kama mtu ananitafuta hawezi kunitafuta kwenye instagram, so may be she is trying to make somebody happy, sasa ndo hicho ambacho kime, umeona labda kuna tatizo.
sijawahi kuwa na matatizo na Ray c mimi hata sijawahi yaani, kwanza sijamuona kama miaka mitano, nashangaa,nini anataka kuongea na mimi Ray C, mbona hajanitafuta miaka yote anitafute saa hivi, if she wanna make a point out of it, i really dont like it yaani wewe sasa nakwambia jamaa hataki kuonana na wewe you drug addicted, you been doing alot of shit, you been staying in ghettos, you been being a prostitute, so me i don't want influence yangu ikawa mbaya, kwahiyo staki kuongea nae staki kukutana nae, akaongee na ma boyfriend zake anaofanya nao vitu vibaya, am not her type, mimi am living with my family, am living with my mum, i drive my cars, come on man,
am not her type, umeelewa, she wants to prove a point, may be she wants to make up with me, am not ready my friend, i don't date women like her, umeelewa, yaani kama anataka back up, asitafute backup kwangu, kuna society kibao ambazo anaweza kuzisaidia, anaweza akashuka pale kinondono manyanya akafanya nini, kwa hiyo she shouldn't be involved na mambo yangu na maisha yangu, awasaidie watu wengine, mimi i really don't need to see her kabisa, she is a bad influence " amesema TID
its more about music industry and social issues in and out of bongo land
Beyonce Knowles aongoza orodha ya watu 100 waliongiza mkwanja na maarufu duniani
Beyonce Knowles, ameongoza nafasi ya kwanza katika list ya watu 100 maarufu duniani kwa mujibu wa Forbes
Forbes wamefanikiwa kutengeneza list hiyo baada ya kufatilia mkwanja walioingiza tangu June 2013 mpaka June 2014 na pia umaarufu wa watu hao kupitia mitandao ya kijamii, radio pamoja na television kujua ni mara ngapi wamekuwa wakitajwa.
Beyonce amemtoa Oprah kutoka katika nafasi hiyo ya kwanza ambayo aliishika mwaka jana, na kumpeleka mpaka nafasi ya nne mwaka huu, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na mcheza kikapu Lebron James.
mwaka wa mafanikio makubwa sana kwa Beyonce hasa kwa tuwa kubwa aliyoifanya, Muimbaji nyota huyo alipiga show 95 na kuingiza wastani wa dola milioni 2.4 kwa kila mji, kwa mujibu wa pollstar.Beyonce pia ameachia album yake mpya "Beyonce" December bila promo yoyote, single "Drunk in love" tayari mpaka sasa imeshauza zaidi ya kupi milioni moja.
Nafasi ya 2 imeshikiliwa na mcheza kikapu Lebron James, 3 ni Dr Dre, nafasi ya 4 imeshikiliwa na Oprah Winfrey, Nafasi ya 5 imechukuliwa na Mtangazaji Ellen Degeneres, huku Jay Z akiwa ameshika nafasi ya 6
Mshkaji wa karibu na 50 Cent, Floyd Mayweather Jr ameshika nafasi ya saba, huku Rihanna akiwa nafasi ya 8, Katy Perry amekamata nafasi ya 9 huku ya kumi ikiwa imehukuliwa na Robert Downey Jr muigizaji wa movie ambae mkwanja mwingi ameingiza mwaka huu kupitia "The Irone Man 3"
its more about music industry and social issues in and out of bongo land
Subscribe to:
Posts (Atom)











